SIKU
ya jana haikuwa nzuri kwa baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia
ya marehemu Deo Filikunjombe baada ya mdogo wake Phillip Filikunjombe
kushika nafasi ya pili katika kura za maoni ya ubunge wa jimbo la Ludewa
zilizofanyika jana, mjini Ludewa.
Uchaguzi
wa ubunge katika jimbo hilo uliahirishwa baada ya aliyekuwa mgombea wa
jimbo hilo, Deo Filikunjombe kufariki dunia katika ajali ya helikopta
iliyotokea Oktoba 15, siku 10 kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu.
Phillip
Filikunjombe aliyekuwa anategemewa na wengi kushinda kura za maoni za
jimbo hilo ili aingie moja kwa moja katika kinyang’anyiro cha ubunge wa
jimbo hilo lililoongozwa na kaka yake Deo katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita, amepata kura 501 akizidiwa na Deo Ngalawa aliyepata
kura 537.
Filikunjombe
aliangushwa na mgombea mwenzake huyo katika kinyang’anyiro
kilichoshikilisha wagombea saba, baada ya wengine watatu kujitoa kwa
ombi la kumuunga mkono Filikunjombe.
Waliojitoa
katika kinyang’anyiro hicho kilichomshilikisha msanii wa vichekesho na
muimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la
‘Masanja Mkandamizaji’ aliyeambulia kura 19 ni pamoja Johnson Mgimba na
Simon Ngatunga.
Wengine
walioshiriki kura hizo za maoni na kura zao kwenye mabano ni James
Mgaya (72), Dk Evaristo Mtitu (21) na Zephania Chaula (21) na Mpangala
Mpangala (3).
Post a Comment