Omari Kigoda
[TANZANIA] Baadhi ya wanachama Chama cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Handeni Mkoani Tanga pamoja na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo wamesikitishwa kwa hatua ya Chama hicho kumpitisha Omari Kigoda (pichani) kuwania Ubunge ndani ya CCM katika kinyang’anyiro cha kuziba nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha Baba yake mzazi marehemu Dkt. Abdallah Kigoda.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka Handeni baadhi ya wana CCM wamesikitika kwa hatua hiyo ya kupitishwa kwa jina la Omari Kigoda huku wakieleza kuwa hana ushawishi wa kisiasa na hali ambayo inaweza kusababisha jimbo hilo kwenda kwa wapinzani ama kulipoteza kama ilivyotokea kwa maeneo mengine ikiwemo Iringa Mjini na Arumeru.
Wakizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu baadhi ya wana CCM hao wamesema kuwa kitendo cha wajumbe wa CCM kumpitisha mtoto huyo ni kulipa fadhila za kununuliwa pikipiki na marehemu Kigoda hivyo waliamua kukaa wenyewe na kumpitisha huku wakiacha utaratibu wa wa kidemokrasia ikiwemo wagombea waliowahi kuchuana na marehemu kigoda katika kura za maoni ndani ya chama.
Baadhi ya mambo ambayo wanalalamikia kuwa licha ya kumpitisha mtoto huyo, hana ushawishi kwa wananchi kwani ndani ya jimbo hilo kumekuwa na kero mbalimbali ikiwemo suala la maji safi na salama pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo.
“Kigoda ametawala Handeni kwa miaka mingi. Kuna alivyofanya na kuna alivyoshindwa. Sasa leo hii wajumbe wa matawi kuamua tu kupitisha jina la Omari Kigoda ni kutuvunjia heshima sie wenye chama chetu kwani hatujatendewa haki” amebainisha mwana CCM huyo mkazi wa Handeni ambaye hakutaka jina litajwe.
Mbali na mkazi huyo kupitia mitando ya kijamii ikiwemo facebook na magroup ya whatsapp na mengine watu mbalimbali wametoa maoni yao kushangazwa na tukio hilo kwani wameliona ni CCM wanataka kupoteza jimbo hilo kama Kamati kuu watampitisha.
Pia wapo waliohoji wagombea 12, waliogombea awali katika kura za maoni na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Kigoda, kuwa ilitosha kuwachuja wagombea hao kwani walifuata vigezo vyote tofauti na mtoto wa Kigoda ambaye amepitishwa na watu wachache wenye maslahi yao binafsi.
NB: Habari hizi ni kwa mujibu wa vyanzo vyetu mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii na baadhi ya wananchi walioongea na mtandao huu mapema leo.
Pia kama una habari ama tukio lolote nawe waweza kututumia kupitia Whatsapp +255767076376 au barua pepe na namba za simu za hapo juu.
Uchaguzi wa jimbo hilo la Handeni unatarajiwa kufanyika hapo baadae kufuatia kusimama baada ya aliyekuwa Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Abdallah Kigoda, kufariki dunia Oktoba 12, nchini India alipokiwa akiendelea kupatiwa matibabu.
Post a Comment