Mtandao
wa wanawake wa Katiba na Uchaguzi wamelaani kitendo cha baadhi ya
wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuuliza maswali
ya kejeli na kumzomea Naibu Spika Wa Bunge, Dokta Tulia Ackson na
kuudhalilisha utu wa mwanamke wakati akijieleza kabla ya kupigiwa kura
na kuidhinishwa na Bunge.
Wamesema
kitendo hicho ni cha udhalilishaji na aibu kufanywa ndani ya chombo
kikubwa cha uamuzi na baadhi ya wabunge ambao ni wawakilishi wa
wananchi.
Akizungumzia
kitendo hicho ambacho kimefanywa na baadhi ya wawakilishi wanaotegemewa
kuwatetea wananchi Mjumbe wa mtandao wa wanawake na Katiba, Dr. Ave
Maria Semakafu amesema kitendo hicho siyo cha kiungwana na wala hakina
maana yoyote kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Vitendo
vya udhalilishaji wanawake wanapogombea nafasi za uongozi visipokemewa
na kuchukuliwa hatua vinatajwa kuwa kikwazo cha malengo endelevu ya
maendeleo ya kuweka usawa wa kijinsia katika ngazi za uamuzi kwa
asilimia 50 kwa 50 kama wanavyobainisha baadhi ya wahariri wa vyombo vya
habari.
Suala la wabunge wa viti maalum nalo likaibuliwa ambalo linatajwa kuondoa ushindani wa wanawake na wanaume kwenye majimbo.
Amesema
viti maalum vimekuwa vikiwanyima wabunge hao baadhi ya stahiki zao kama
wabunge ikiwa ni pamoja na kuchaguliwa katika baadhi ya nafasi za
uongozi na fungu la kuwawezesha kufanya maendeleo kwa wananchi.
Wakijadili
masuala mbalimbali ya kiharakati katika kutetea haki za msingi za
wanawake nchini, wanaharakati hao kutoka TGNP, TAMWA na ULINGO wameitaka
ya awamu ya tano kutekeleza ahadi zake za kumkomboa mwanamke kutoka
kwenye lindi la umasikini pamoja na kutatua changamoto za afya ya uzazi,
maji na ukatili wa kijinsia bila kuacha upatikanaji wa Katiba Mpya.
Post a Comment