Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la bunge
WABUNGE
wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamepanga
kuchanga Sh. 33.9 milioni kwa ajili ya kusaidia familia ya aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani wa
Geita, Alfonce Mawazo.
Fedha,
hizo zimepatika baada ya wabunge 113 wa Ukawa kuchangishana kiasi Sh.
300,000 kila mmoja ambazo zitakabidhiwa familia ya Mawazo ambaye ameuawa
kikatili na watu ambao mpaka sasa hawajabainishwa.
Mwenyekiti
wa Chadema – Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman
Mbowe alisema hayo wakati akizungumza mjini hapa Dodoma kuhusu
maandalizi ya mazishi ya kada huyo ambaye anatajwa kuwa shujaa katika
mapambado ya kutafuta ukombozi Ukawa.
Mbowe
amesema licha ya kwamba Mawazo alikuwa mwanachama wa Chadema lakini pia
alishiriki vyema katika ukombozi ndani ya Ukawa kwa kutetea masilahi ya
Watanzania kwenye mkoa wake wa Geita pamoja na mikoa mingine nchini.
“Kwa
ujumla wetu wabunge takribani 113 tumekubaliana kuchanga kiasi cha Sh.
300,000 kila mmoja kwa ajili ya kuiwezesha familia yake ambayo ameiacha.
“Kumbuka
kwamba Mawazo amepigania masilahi ya Watanzania wengi katika mkoa wake
wa Geita lakini pia katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
“Hivyo
tunalazimika kumuenzi ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wetu wa
Ukawa na ikumbukwe kuwa, kwa sasa seriali ya CCM inaonesha wazi kutumia
vyombo vyake vya dola kudidimiza upinzani,” amesema Mbowe.
Hata
hivyo, Mbowe amesema inasikitisha kuona jeshi la polisi linavyotumiwa
vibaya na kujikuta linafanya kazi za siasa badala ya kusimamia ulinzi na
usalama wa raia.
“Leo
(juzi), baada ya viongozi wa Mji wa Mwanza kupambana vikali na Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, aliwaambia viongozi wa Chadema kuwa
intelejensia imeonesha kuwa, iwapo watafanya mkusanyiko wa ibada kuna
uwezekano wa kuzuka machafuko.
“Baada
ya kupata taarifa hizo nilipata kuzungunza na IGP na kuniahaidi
kunipatia majibu lakini hadi sasa sijafanikiwa kupata majibu lakini
jambo lingine na la ajabu ni pale ambapo wamegeuza kibao na kusema
hakuna kufanya ibada kwani kwa sasa kuna ugonjwa wa kipindupindu hivyo
hakuna mkusanyiko,” amesema Mbowe.
Mbowe
amesema lazima Watanzania watambue kuwa serikali inatumia vibaya vyombo
vyake vya dola kuzuia wapinzania wasifikishe ujumbe wao kwa jamii,
imekifia hatua ya kuzuia hata watu kuwazika wafuasi wao.
“Sasa
angalia kutuuwa wanatuuwa lakini hatua ya kutunyanyasa na kukataa hata
tusimzike mtu wetu jambo hilo ni la ajabu sana lakini najua tutafikisha
ujumbe kwa njia nyingine ambayo inafaa na kwa ustaarabu,” amesema Mbowe.
Post a Comment