Polisi
mkoa wa Mwanza imezuia mikusanyiko ya watu na maandamano kwa kuhofia
kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu ambao unatajwa kuzagaa mkoani humo.
Hatua
hiyo inatokana na kuwepo kwa taarifa za shughuli ya kuuaga mwili wa
aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa
wa Geita katika viwanja vya Furahisha.
Kwa
mujibu wa taarifa za kiintelijensia za jeshi la polisi, mwili wa
aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Alphonce Mawazo
unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Licha
ya marufuku hiyo, Jeshi la polisi limeahidi kushirikiana na
waombolezaji kuhakikisha mwili huo unafikishwa kwa amani mkoani Geita
Katika
hatua nyingine, Kamanda Mkumbo amesema tarehe 16 mwezi huu kuliripotiwa
mvua kubwa wilayani Kwimba ambayo ilisababisha kifo cha mzee wa miaka
80, na nyumba 300 kuharibiwa na mvua.
Kaimu
mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza Onesmo Ruwakendwa amewataka wananchi
kutii amri ya kutokukusanyika na kufanya maandamano ili kuepusha
maambukizi mapya ya ugonjwa wa kipindupindu.
Mkoani
Mwanza Ugonjwa wa kipindupindu uliripotiwa kuanza miezi miwili
iliyopita na hadi sasa wagonjwa 420 wamelazwa na 28 tayari wamepoteza
maisha.
Post a Comment