Aaliyekuwa Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa leseni ya chama cha ACT-
Wazalendo, Seleman Abdallah Msindi ‘Afande Sele’.
Dustan Shekidele, Mororogoro
ALIYEKUWA Mgombea Ubunge wa Jimbo la
Morogoro Mjini kwa leseni ya chama cha ACT- Wazalendo, Seleman Abdallah
Msindi maarufu kama Afande Sele, ameburuzwa mahakamani akidaiwa kutapeli
fedha zilizotokana na kuchapishiwa fulana zilizotumika wakati wa
uzinduzi wa kampeni zake Septemba 14, mwaka huu.
Hellen B Massawe
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni msanii
mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya, amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo
Chamwino akidaiwa kutomlipa mjasiriamali Hellen B Massawe kiasi cha
shilingi 1,390,000.
Hellen ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam,
aliliambia gazeti hili akiwa nje ya ofisi za chama hicho mjini Morogoro
kuwa alikopa benki na kufanya kazi ya kutengeneza fulana hizo kwa
wanasiasa wa vyama vingi, lakini ni Afande Sele pekee ambaye hakumlipa
na kila alipomfuata alimtaka kufuata fedha hizo kwa kiongozi mkuu wa
chama, Zitto Kabwe.
“Baada ya kuzunguka huku na kule bila
mafanikio, hasa baada ya kuambiwa kuwa chama kisingeweza kumpa fedha kwa
vile mgombea huyo alishapewa ruzuku, aliamua kwenda mahakamani kufuatia
ushauri wa polisi kuwa hiyo ni kesi ya madai. Nimeenda mahakamani na
nikapewa samansi ambayo Afande Sele ameisaini,” alisema.
Katika
uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, Aziz Abood alishinda
Ubunge Jimbo la Morogoro mjini kupitia CCM huku mgombea wa Chadema,
Marcossy Albani akishika nafasi ya pili na Afande Sele aliambulia nafasi
ya tatu.
Post a Comment