Msanii wa filamu nchini Tanzania, Jacqueline Wolper, aliyekuwa mstari wa mbele kumsapoti mgombea urais kwa mwavuli wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa, amedai kuwa kwake yeye mheshimiwa huyo ndiye kiongozi shupavu na jasiri.
Wolper,
amemmwagia sifa lukuki waziri mkuu huyo wa zamani na kuwataka
Watanzania kuwa pamoja katika kuijenga nchi na kudai kuwa Mh. Lowassa
amekuwa mstari wa mbele kwa kupambana kwa kuleta mabadiliko kwa
watanzania.
Amenukuliwa
akisema kuwa anaamini kuwa Lowassa, ameleta historia kubwa sana nchini
kwasababu haijawahi kutokea Tanzania, kwani ametuma ujumbe kwa viongozi
wengine ambao walikua wazembe na waliojisahau na kudai kuwa anaamini
wataifanya nchi kuwa mpya.
Ameongeza
kuwa yeye bado anaamini Lowassa ni kiongozi shupavu, muelewa na mwenye
akili za kupambanua mambo, na kusema kuwa kushindwa kwake haijalishi kwa
sababu anaamini watanzania wanamkubali hasa kwenye mabadiliko.
Aidha,
amewataka wasanii wenzake ambao wapo CCM wasijengeane chuki kwa
yaliyotokea kwani aliamua kutafuta haki yake ya msingi akiwa kama
msanii.
Sambamba
na hilo amedai kuwa kwa wana mabadiliko wenzake waendelee kupambana na
watakao wawakilisha bungeni wafanye kazi ya maana hasa kuwatetea
wanyonge.
Post a Comment