Hatimaye
Alikiba ametoa wimbo wake “Lupela” uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki
wake Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa. Wimbo huo ni sehemu ya
kampeni ya “Ujangili Unatuumiza Sote” iliyozinduliwa mwaka jana na
WildAid na African Wildlife Foundation mashirikia yanayofanya kazi
pamoja barani Afrika na Asia kupunguza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na
wanyamapori na kuongeza uelewa wa janga la ujangili linaloikabili
Afrika. Video
ya wimbo huo imerekodiwa jijini Los Angeles Marekani ambapo Alikiba
alikuwa mgeni rasmi kweye hafla maalum iliyoandaliwa na shirika la
uhifadhi wanyamapori la kimataifa la WildAid. Chini ya kauli mbiu
“Ujangili Unatuumiza Sote”, Alikiba amefanya kazi na WildAid kuongeza
uelewa wa Watanzania kuhusu tatizo la ujangili wa tembo ambao
wamechinjwa kwa maelfu miaka ya hivi karibuni kwa ajili ya meno yao.
Katika
uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Slipway jijini
Dar es salaam, wageni mbalimbali na waandishi wa habari walipata fursa
ya kuusikiliza wimbo na kuangalia video yake kwa mara ya kwanza.
"Tunaona fahari sana kuwa na Alikiba kama Balozi wa WildaAid”, alisema
Salome Gasabile Meneja wa WildAid Tanzania. “Katika mwaka mmoja
uliopita, yeye na meneja wake Seven wamefanya kazi bila kuchoka kupinga
ujangili wa tembo na tunaamini wimbo huu utakuwa na faida kubwa katika
vita dhidi ya ujangili”. “Nina furaha kubwa kuwa sehemu ya mradi huu.
Naamini kila mara watu wakisikiliza wimbo huu watakumbuka faida ya tembo
kwa urithi na uchumi wa bara la Afrika. Wanaingiza pesa nyingi kupitia
utalii na fedha hizo zinaweza kusaidia kuleta ajira, kujenga shule na
hospitali kwenye jamii zinazozunguka hifadhi za taifa,” alisema Aleya
Aleya Janell ambaye ameshiriki kwenye video ya wimbo huo kama Lupela.
Asha
Franklin, aliyeshiriki kama tembo wanaocheza muziki amefanya kazi na
Rihanna na Ciara katika video mbalimbali amesema “Hii video ni nzuri
kwani imechanganya burudani ya muziki na jambo zuri kwa jamii” Ushiriki
wetu kama tembo wananocheza muziki ilikuwa ni ubunifu wa hali ya juu
lakini pamoja na kwamba ni burudani bado unaweza kuona faida ya kubwa ya
wimbo huu.” Video hiyo iliongozwa na Kevin Donovan, huku ikirekodiwa na
kutengenezwa na muandaaji filamu maarufu wa Hollywood Brian Rumsey
ikiwa ni mchango wake kwa kampeni hiyo. Oththan Burnside, ambaye
ameishafanya kazi na wanamuziki wengi maarufu kama Rihanna na Sean Paul
alihusika kuandaa wimbo huu na staili ya uchezaji wa tembo.
“Tuufanye
mwaka 2016 mwaka wa tembo – mwaka ambao hatimaye tutakumbuka kuwa
hatimaye tuikomesha ujangii wa tembo na kuwapa tembo nafasi ya kuishi”
alisema Burnside. “Tusaidie kuokoa maisha ya wanyama hawa wazuri,”
alisema Burnside. Kwa mujibu wa shirika la WildAid wimbo huo hautatumika
kibiashara na unapatikana bure kwa mashabiki kupakua au kusikiliza
kweye mtandao wa www.yearoftheelephant.org Uzinduzi wa wimbo huo umeenda
sambamba na kampeni ya #jointheherd inayofanyika kupiti mitandao ya
kijamii ikiongozwa na wau maarufu mbalimbali wakiwemo muigizaji Lupita
Nyong’o, Jackie Chan na Jacqueline Mengi ambao wanaendelea kuhamasisha
watu kupitia www.yearofthelephant.org ambapo watu huweza kujitengenezea
picha zao na kuzitumia kwenye mitandao ya jamii.
Post a Comment