Shimo katika tuta la reli eneo la Buguruni kwa Mnyamani ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.
KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni
ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari
09, 2016.
Taarifa
imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua
kuchimba shimo kubwa katika tuta la reli karibu na stesheni ya Buguruni
kwa Mnyamani.
Uharibifu
huo uligundulika leo asubuhi mara baada ya treni kupita eneo hilo
ikielekea stesheni ya Dar es Salaam.wakati wa safari yake ya kwanza
kutoka Kituo cha Ubungo Maziwa.
Tayari
mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakiendelea na kazi ya
ukarabati na kwamba inatarajiwa huduma hiyo itarejea tena hapo kesho
kama kawaida.
Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.
Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Nd Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,
Februari 09, 2016.
Post a Comment