Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CHAMA CHA ACT WAZALENDO WAMKOMALIA JECHA ... WATOA MSIMAMO MKALI

ACT-Wazalendo
TAARIFA KWA UMMA:
Tumekuwa tukipokea simu za waandishi mbali mbali baada ya kauli ya jana ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),Jecha Salum Jecha kuwa hakuna chama kilichojitoa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu.
 
Msimamo wa ACT-Wazalendo ni kuwa hatutashiriki Uchaguzi huo kama ilivyoazimiwa katika kikao cha kamati kuu cha february 14 mwaka huu
Hatushiriki kwa kuwa tunaamini kuwa hakuna sababu ya kufanyika uchaguzi mwingine nje ya ule uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana
 
Taarifa hii ya kutoshiriki uchaguzi wa machi 20 mwaka huu imewasilishwa katika ofisi ya ZEC Zanzibar february 9 mwaka huu baada ya wao kututaka tuthibitishe kwa maandishi kama tutashiriki au la
 
Hivyo kauli ya Jecha kuwa hakuna chama kilichofuata utaratibu ni muendelezo mwingine wa kutaka kuhalalisha haramu kuwa halali kama walivyofanya katika kufuta uchaguzi wa Oktoba 25
Kwa kuthibitisha dhamira yetu hii ya kutoshiriki hivi karibuni kamati Maalum ya uongozi Zanzibar ilimsimamisha uanachama ndugu Khamis Idi Lila,aliyedhaminiwa na chama kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi uliofutwa kwa "Zengwe" hivyo hatuna mwanachama anayewania nafasi hiyo
Jecha amezungumzia Sheria ya Uchaguzi na wajibu wa mgombea aliyedhaminiwa na chama 
kuthibitisha ushiriki wake,huku akiacha kwa makusudi kuainisha udhamini huo ni katika uchaguzi gani
ACT-Wazalendo haijamdhamini mwanachama wake yeyote kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Machi 20 na hili lilipewa msisitizo katika kikao cha kamati kuu iliyofanyika february 14 na taarifa kutolewa kwa umma siku iliyofuata
 
Tunaomba wananchi wapuuze ulazimishaji huu wa ZEC kwa kutaka kuionesha dunia kuwa vyama vimeshiriki uchaguzi huo haramu.
 
ACT wazalendo katika kikao chake cha kamati kuu iliazimia kuwa haitakuwa muhuri wa kuwasafisha wabakaji wa Demokrasia kwa kushiriki uchaguzi wa Machi 20
Abdallah Khamis
Afisa Habari

ACT Wazalendo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top