Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAAMUZI YA NRA JUU YA MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR HAYA HAPA ..

  Katibu Mkuu Chama cha NRA Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya (wa pili kushoto) akitoa tamko la chama chake kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar March 20 ya waandishi wa Habari(Hawapo Pichani)leo Jijini Dare s salaam katika ukumbi wa Habari Maelezo.

Baaadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano ulioitishwa na Chama cha NRA kuelezea ushiriki wao katika uchaguzi wa marudio Zanzibar.
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO


Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) kutoka Zanzibar kimethibitisha kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu baada ya kikao kilichofanyika Februari 15.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Tanzania Bara Hassan Almasi Kisabya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa Chama hicho kitashiriki uchaguzi wa marudio na kusisitiza kuwa tamko lililotolewa na mgombea wao la kutoshiriki uchaguzi wa marudio lipuuzwe kwani ni tamko lake binafsi na sio msimamo wa chama.

“Tamko lililotolewa tarehe 14/02/2016 Si Tamko la chama cha NRA bali ni tamko binafsi na wale waliomuagiza kwani yeye hana mamlaka ya kukisemea chama wala wagombea wengine wa chama pasipo Baraka na vikao halali vya chama” alisema Kisabya.

Amesisitiza  kuwa maamuzi ya chama ni sharti yatoke katika chama na sio kwa mgombea na ikiwa yeye amejitoa anatakiwa afuate taratibu za kisheria katika kujitoa kama alivyofuata sheria katika kugombea nafasi hiyo.

Aidha, Chama kinatoa taarifa kwa wagombea wote Zanzibar kujiandaa na wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu ili kutimiza haki yao kikatiba na kuchagua viongozi wao kwa kipindi cha miaka mitano ijayo

Chama cha NRA ni miongoni mwa vyama 14 vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa  Oktoba 25 mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofutwa kwa nafasi ya Rais.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top