Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MBUNGE 'PROFESA JAY' AGAWA MISAADA ZAIDI JIMBONI KWAKE

Mbunge Professor Jay atoa msaada kwa Kaya zilizoathirika na Mafuriko.

Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni mwanamuziki wa Hip Hop Tanzania, Joseph ‘Prof Jay’ Haule, ametoa msaada wa chakula kwa wananchi waliokumbwa na hadha ya mafuriko kata ya Tindiga jimboni humo.
Katika mafuriko hayo, nyumba zaidi ya 600 zimeharibiwa na watu zaidi ya 5060 wameathirika na mafuriko hayo.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, ameweka bayana kuwa ametoa tani 1 ya unga, maji lita 13000, Maharagwe, mafuta na dawa za mbu.
“Ndugu zetu wa kata ya Tindiga wamepata maafa ya mafuriko makubwa sana na mpaka sasa nyumba 600 zimeanguka, kaya zaidi ya 1300 zimeathirika sana na watu 5060 wanahitaji hifadhi,
Mimi kama mbunge nimepeleka tani moja ya unga, maji lita 13,000, Maharage, Mafuta ya kupikia, chumvi na dawa za mbu nk
Bado ndugu zetu wanahitaji sana msaada zaidi ili waweze Kukabiliana na hali ngumu wanayokutana nayo…
Mahitaji ni Maji, Chakula, Mahema, chandarua na dawa za mbu nk
MUNGU AWABARIKI SANA!!!!” ameandika.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top