Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MREMA AIBUKA NA KALI ... NI JUU YA MIUJIZA YA MAGUFULI

Mwanasiasa Mkongwe, Augustine Mrema amemuelezea Rais John Magufuli kama kiongozi wa Tanzania anayetenda miujiza kutokana na utendaji wake ndani ya siku 100 tangu alipoingia madarakani.

Mrema ambaye alikuwa mbunge wa zamani jimbo la Vunjo na kuangushwa kwenye uchaguzi uliopita na James Mbatia (NCCR – Mageuzi), aliendelea kuutetea uamuzi wake wa kumpigia debe Dk. Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ingawa chama chake cha TLP kilikuwa kimesimamisha mgombea urais.

“Nilijua wazi Rais Magufuli ni mtendaji ndio maana hata wananchi waliponiadhibu kwa sababu ya kumpigia debe sikuumia, najivunia chaguo langu na kiukweli anafanya miujiza ya hali ya juu,” alisema Mrema.

Mrema ambaye ni mwenyekiti wa TLP, alimuelezea Magufuli kama kiongozi mwenye uthubutu huku akiwataka watanzani kuacha unafiki na kumpa nafasi zaidi ya kufanya kazi
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top