Mkurugenzi
wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo
jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi.
Ruth Minja.(Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo)
Meneja
wa Takwimu za Bei na Ajira toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth
Minja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei mapema hii leo jjijjini Dar es
Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo.
Mkurugenzi
wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
Ephrahim Kwesigabo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) wakati akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa beimapema hii leo
jijini Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi.
Ruth Minja.
Na; Frank Shija, MAELEZO
Matumizi
ya kaya kwenye biadhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka
2011/12 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007.ambapo kwa ujumla wake
mfumuko wa Bei umepungu
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu kutoka
Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizunguza na
waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam.
Kwesigabo
alisema kuwa kutokana na mwenendo huo kunaashiria kupungua kwa
umasikini wa kipato kwenye kaya kwa kuelekeza matumizi mengine bidhaa
zisizo za vyakula kama usafiri, mawasiliano, makazi, maji na nishati.
“Matokeo
yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula
imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 mwaka
2007” Alisema Kwesigabo.
Aliongeza
kuwa makundi mengi mengine yaliyoonyesha kuwa na mizania mikubwa ya
matumizi ya kaya mwaka 2011/12 kuwa ni pamoja na Usafi asilimia 12.5
kutoka asilimia 9.5 mwaka 2007, Makazi Maji na Nishati asilimia 11.6
kutoka asilimia 9.2 mwaka 2007 na Mavazi na Viatu asilimia 8.3 kutoka
asilimia 6.7 mwaka 2007.
Aidha
kumekuwa na ongezeko la Zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye
kundi la Mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya
mwaka 2007
Kwa
upande wake Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Bibi. Ruth Minja amevitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika
kupata Fahirisi za Bei zinzoonyesha uhalisia wa matumizi ya kaya
binafsi kuwa ni pamoja na mizania katikia bidhaa na huduma muhimu
ikiwemo Vyakula, afya, Usafiri ,Maji na Nishati.
Aliongeza
kuwa ili kupata matokeo ya mfumuko wa Bei kumekuwa na mtindo wa kufanya
marejeo baada ya kila miaka mitano ambapo marejeo ya mwisho yalifanyika
mwaka 2007 na kuonyesha matumizi makubwa ya kaya yalikuwa kwenye bidhaa
za vyakula zikiwa na asilimia 47.8 ya matumizi yote yakifuatiwa na
usafiri asilimia 9.5 huku matumizi madogo zaidi yalikuwa ni huduma za
afya kwa asilimia 0.9.
Takwimu
hizi zimekuwa zikitolewa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015
na zimekuwa zikisaidia katika kupima na kuboresha sera za kifedha na
mipango ya kiuchumi ya kuthibiti mfumuko wa bei, kukadiria pato la
Taifa,kuboresha mishahara ya wafanyakazi na mafao ya wafanyakazi
waliostaafu.
Post a Comment