Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
ameyataka Mabaraza na Bodi za kitaalamu za masuala ya afya kuchukua
hatua za kinidhamu dhidi ya wataalam na vituo vinavyotoa huduma za afya
kinyume cha Sheria.
Waziri
Ummy ametoa agizo hilo alipokuwa akizindua Baraza la Optimetria, Baraza
la wataalamu wa Radiolojia pamoja na Bodi ya Maabara binafsi leo jijini
Dar es salaam.
Alisema
kisheria Mabaraza na Bodi za Kitataalam ndivyo vyombo vinavyofuatilia
ubora wa huduma za Afya pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuwaepuka
watoa huduma batili wasiokuwa na utaalam na ujuzi wala kukidhi vigezo
vya utoaji huduma vilivyowekwa kisheria.
“Siku
hizi kumekuwa na matumizi makubwa ya vyeti vya kugushi vikiwemo vya
vituo vya kutolea huduma na wataalamu, watu wasio na taaluma wanatoa
huduma kinyume na sheria hivyo Mabaraza na Bodi mna mamlaka ya
kuwachukulia hatua za kinidhamu,” Alisema Waziri Ummy.
Aidha,
alisema kuwa Serikali haitasita kuyachukulia hatua kali za kisheria
ikiwemo kuvunja Bodi au Mabaraza yatakayoshindwa kutekeleza majukumu
yaliyoainishwa katika sheria iliyohusika kuyaanzisha.
Aliyataka
mabaraza hayo kuhakikisha kuwa yanatoa Elimu kwa wananchi kupitia
vyombo vya habari ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na ufahamu kuhusu
huduma bora za afya zitolewazo na wataalamu husika.
“Wananchi
wakielimishwa wataepuka watoa huduma batili wasiokuwa na utaalamu na
ujuzi hivyo mabaraza na Bodi vinapaswa kuhakikisha mambo haya
hayatokei kwani vinauwezo mkubwa wa kufuatilia masuala haya kwa mujibu
wa Sheria”alifafanua Waziri Ummy.
Akizungumza
kuhusu utendaji kazi wa wataalamu hao Waziri Ummy amewataka wataalamu
hao kujiendeleza kielimu kwani utaalamu bila kuwa na ujuzi ni butu hivyo
suala la elimu lipewe kipaumbele.
Mbali
na hayo Waziri ameitaka Mabaraza na Bodi kuhakikisha wataalamu wote,
vifaa na vitendanishi vinasajiliwa kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na
Taratibu zilizowekwa.
Post a Comment