Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utumbuaji wa majipu unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano haumuonei mtu, bali ni harakati za kupambana na wanaokwenda kinyume cha taratibu za nchi.
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau uliolenga kutoa taarifa ya hali ya kiuchumi na maendeleo ya mikoa ya Katavi na Rukwa jana, Majaliwa alisema tangu Serikali ianze kuwawajibisha watendaji wazembe kumekuwa kukizuka maneno mbalimbali kwa baadhi ya watu wanaochukuliwa hatua hizo.
“Kaulimbiu yetu ya ‘Hapa Kazi Tu’ inalenga kuwakumbusha wananchi wote kuwajibika kwenye sekta zao ili kila mmoja azalishe na kutunisha pato la Taifa.
“Kipindi cha kampeni tuliahidi kupambana na hali hii, ndicho tunachokifanya ili kila mmoja atambue wajibu wake,” alisema Majaliwa.
Post a Comment