Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba ametembelea Kijiji
cha Kigurukwa mjini Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na
Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi takribani 200.
Waziri Mwigulu
ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katika
tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pia
ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2005
iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima
Post a Comment