Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ZEC YAKOMAA ... YASEMA WAGOMBEA WOTE NI HALALI

Tume ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza kutotambua chama chochote kujitoa katika uchaguzi mkuu wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, kwa madai kuwa hakuna chama kilichofuata kanuni katika kujitoa.

Wakati baadhi ya vyama vya siasa vikitangaza kujitoa uchaguzi wa marudio Zanzibar, Tume ya Uchaguzi visiwani humo ZEC- imetoa msimamao wake na kusema kuwa wagombea wote ni halali na watagombea nafasi zao kwa vile hakuna hata chama kimoja kilichofuata sheria na kanuni za uchaguzi.

Msimamo huo wa tume umetolewa na mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo amesema kuna utaratibu wakujitoa na kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi hakuna chama kilichofuata kanuni ikiwa ni pamoja na wadhamini wa wagombea kutangaza kuondoa udhamini wao, hivyo wagombea wote wa urais, uwakilshi na udiwani wote bado ni halali.

Akizungumzia maandalizi hayo amesema yanaenda vizuri ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wasimamizi wa uchaguzi, upangaji wa vifaa, mawasiliano na vyama na uchapishaji wa daftari na mafunzo na wagombea kuanza kupatiwa ulinzi na haki zote kwa mujibu wa sheria.

Jecha pia amesema kuwa karatasi za kura ambazo zinachapwa nje ya nchi zinatarajiwa kuwasili mapema mwezi ujao.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi vyama ambavyo vimethibitisha kushiriki ni pamoja na CCM, TADEA, ADC, CCK, AFP, SAU, TLP, CUF, NRA, CHAUMA, DP, Jahazi Asilia na ACT Wazalendo ambacho mgombea wake Khamis Lilla ametangaza kugombea huku chama chake kikimufukuza uanachama...
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top