Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.
MBUNGE wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) pamoja na Manase John Mjema wamepandishwa kizimbani leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na kusomewa shtaka la kumjeruhi Theresia Mbaga kwenye ukumbi wa Karimjee mnamo Februari 27 mwaka huu.
Washtakiwa wengine katika shtaka hilo ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima James Mdee, Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mwita Mwikabe Waitara na wengine wawili.
Kubenea na Mjema wote wamekana shtaka na kujidhamini wenyewe baada ya kusaini dhamana ya shilingi milioni mbili kila mmoja.
Post a Comment