Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

DAWASCO YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI

Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji kwenye operesheni yake maalumu ya kubaini watumiaji wa huduma ya Maji ambao hawajaunganishiwa kihalali kwenye mtaa wa Ilala kota karibu na nyumba za Shirika la nyumba la taifa (Nhc) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye tukio hilo Meneja wa Dawasco Ilala, mhandisi Ramadhani Mtindasi alieleza kuwa wanatekeleza agizo la Mh. Waziri wa Maji ambapo amewaagiza Dawasco kufunya uchunguzi kwenye Magorofa yote makubwa jijini ambayo wanadai wanatumia Maji ya visima na ndipo walipogundua jengo hilo la ghorofa lenye nyumba ndogo (apartments) 8 likiwa na laini mbili moja ya Maji ya kisima na nyingine ni ya Dawasco ambayo haikuwa na mita wala kusajiliwa na Dawasco .
“Tumeanza operesheni maalum ya kukagua majengo yote makubwa jijini ambayo wanatumia huduma ya Maji ilikubaini kama ni ya visima au ya Dawasco kama Mh. Waziri wa Maji alivyotuagiza na ndipo tulipogundua jengo moja eneo la Ilala kota likiwa na laini ya Maji ya Dawasco ila halina mita wala hatujamsajili amejiunganishia kiholela”
“Hivyo tuwewashirikisha serikali za mitaa kubaini mmiliki wa jengo hilo lakini hakuweza kufahamika bali tumepata namba zake za simu na tulipompigia alidai anatumia huduma ya Maji ya kisima tu hivyo tumemuandikia barua afike kwenye ofisi zetu kujisali na alipe faini”, alisema mhandisi Mtindasi.
Kwa upande wa mjumbe mtaa wa Ilala Kota Bi Habiba Hamisi ameeleza kuwa Majengo mengi makubwa yamekuwa yakijiunganishia huduma ya Maji kiholela na kudai kuwa ni ya kisima kumbe sio hivyo kuwafanya wananchi wengine waotegemea huduma ya Maji ya Dawasco kukosa kutokana na kuwa majengo hayo makubwa yana matumizi makubwa.
“Majengo mengi makubwa yana laini mbili ya Dawasco na visima ila ukiwauliza wasema wanatumia maji ya visima tu kumbe sio kweli na matumizi yao kwenye majengo hayo ni makubwa hivyo wanasabisha wanaostahili kukosa huduma ya maji hivyo Dawasco wawachukulie hatua kali za kisheria” alisema Bi Hamisi.
Dawasco imewasihii wamiliki wote wa majengo makubwa ambao wamejiunganishia huduma ya Maji Kiholela kujisalimisha mapema kabla ya hatua kali za kisheria hazijachukuliwa juu yao endapo watakamatwa. 
 Meneja wa Dawasco llala (katikati) Mhandisi Ramadhani Mtindasi pamoja na mjumbe wa mtaa wa Kota Bi. Habiba Hamisi akionyesha bomba la Maji ambalo linaleta Maji kutoka kwenye laini kuu lilo uunganishwa kiholela inayotoka kwenye Bomba kubwa kwenye eneo la Ilala Kota Mchikichini Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Dawasco Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi  akionyesha boza linalotumika kuhifadhi Maji yanayotoka kwenye bomba la Dawasco .
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top