Mbunge wa Bunda mjini.Ester Bulaya amewasili jijini mwanza usiku huu baada ya kuhojiwa kwa masaa matatu jijini Dar na kikao cha kamati ya haki, kinga na madaraka ya bunge.
Bulaya alikamatwa usiku wa manane wa kumkia leo kwa amri ya spika wa bunge ambapo alisafirishwa hadi jijini Dar es Salaam kwa ndege kujibu tuhuma zinazomkabili.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya kurejea jijini Mwanza usiku huu, Bulaya amesema anashangazwa na kitendo cha serikali kutumia pesa na nguvu nyingi kumkamata wakati pesa hizo zingeweza kutumika kuboresha maisha ya askari polisi
Post a Comment