Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIGOGO BOT ASAFISHWA ESCROW


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeyafuta mashtaka ya kupokea rushwa ya mamilioni ya fedha  kutoka kwa mfanyabiashara James Rugemalira, yaliyokuwa yakimkabili   Mkurugenzi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Julius  Rutta  Angello.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi jana alimfutia Angello mashtaka hayo yaliyokuwa yakimkabili baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maxi Ali  kudai kuwa hawana nia ya kuendeleza mashtaka hayo.

Kesi hiyo ambayo ilikuwa imefikia hatua ya usikilizwaji wa awali, Ali alimweleza Hakimu Shaidi kuwa ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na kwamba, wana shahidi mmoja  lakini hawana nia ya kuyaendeleza mashtaka hayo na kuomba yaondolewe kortini chini ya kifungu cha 98 (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Shahidi alikubaliana na Ali hivyo kumfutia mshtakiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

Angello anadaiwa Februari 6, 2014 maeneo ya Benki ya Mkombozi, akiwa Mkurugenzi wa Fedha wa BoT alipokea rushwa ya Sh 161.7 milioni kupitia akaunti namba 00120102646201 kutoka kwa James Rugemalira.

Fedha hizo zinazodaiwa  zilikuwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow, alipokea kama tuzo kutokana na malipo yaliyotolewa katika akaunti hiyo kwenda Pan Africa Solutions Limited (PAP).

Mshtakiwa  huyo alikana shtaka, upelelezi ulikuwa umekamilika  na akaunti yake hiyo inayodaiwa kutumika kupokea fedha hizo ilizuiwa na mahakama kwa muda, mtu yeyote hakuruhusiwa kufanya kitu chochote kwenye akaunti hiyo. Alikuwa nje kwa dhamana.

Mshtakiwa huyo alikuwa nje kwa dhamana baada  ya kukamilisha masharti aliyopewa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top