Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amewapa neno wanachama wa CCM wanaotaka kufukuzwa ndani ya chama hicho wakituhumiwa kumuunga mkono.
Akiongea hivi karibuni katika kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kilichofanyika jijini Mwanza, Lowassa aliwasihi watu hao kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema kwani kuna maisha mazuri zaidi ndani ya chama hicho kikuu cha upinzania.
“Lakini hivi karibuni kuna utaratibu wa kuwafukuza kwenye chama watu ambao waliniunga mkono. Wanafukuzwa wanaambiwa ‘ondokeni mfuateni Lowassa’.
"Nasikia kuna mipango mikubwa zaidi baada ya mwezi wa sita atakapokabidhiwa Rais Magufuli… kuna mipango mikubwa zaidi ya kuwaondoa kwenye chama,” alisema Lowassa.
“Sasa mimi nawaambia kwa niaba yetu. There is life outside CCM, nawaambia tena kwa ajili yenu, waje Chadema kuna maisha mazuri tu hapa. Wasibaki huko wananyanyaswa, wanabezwa wanafanya nini… waje tushirikiane tufanye kazi,” aliongeza.
Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa CCM hivi sasa wanaumia kwa sababu kuondoka kwake na kujiunga na Chadema kuliiongezea nguvu kambi hiyo ya upinzani na kupunguza ruzuku kwa kiasi kikubwa kwa chama hicho tawala.
==> Msikilize Lowassa hapo chini akiongea
Post a Comment