HALMASHAURI ya Wilaya ya Monduli imewasimamisha kazi watumishi watatu wa idara ya Ardhi Wilayani humo kwa tuhuma za wizi wa fedha za viwanja na uuzaji wa viwanja bila kufuata taratibu na kuisababishia Halmashauri hasara ya zaidi ya shilingi milioni 700.
Akitangaza maazimio hayo mbele ya kikao cha baraza la madiwani mara baada ya kukaa kama kamati mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Isaack Joseph amesema maamuzi yote hayo ni kuhakikisha wanarejesha nidhamu ya utumishi serikalini na kuunga mkono jitihada za Rais kurejesha nidhamu kwa watumishi wa Umma.
Aliwataja watumishi ambao wamekumbwa na maamuzi hayo kuwa ni Leonard Haule mpimaji ardhi, Kitundu J. Mkumbo Afisa ardhi mteule na Leoni Mkwavi mrasimu ramani ambapo wanadaiwa kuuza viwanja na fedha kutoziwasilisha Halmashauri na pia baadhi ya viwanja walivyouza kutoviingiza katika ramani ya Halmashauri.
Halmashauri hiyo pia kupitia baraza la madiwani wameazimia kwa pamoja kumuomba Rais Magufuli kuitupia macho idara ya Temesa mkoani Arusha na kuamua kwa kauli moja kutopeleka vifaa na magari yao katika taasisi hiyo ya serikali kwa ajili ya matengenezo kutokana na gharama kubwa wanazotoza.
Maamuzi hayo mazito ya madiwani wa Halmashauri ya Monduli yamefanywa katika kikao chao cha kwanza cha baraza la kawaida la madiwani pamoja na maamuzi hayo kilipokea taarifa mbalimbali zakamati kwa robo mwaka ya octoba hadi desemba 201
Loading...
Post a Comment