Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi amedai kuwa walipotangaza kuufungia wimbo huo walipokea malalamiko ambayo hawajawahi kuyapata.
“Wimbo huu ulikuwa kwenye demand kubwa, yaani ukimwambia mtu autoe huu wimbo ni issue na umeona reaction ya watu,” Mungi alisema kwenye mkutano maalum kati ya mamlaka hiyo na AY wiki hii.
Hata hivyo alimuomba AY kutochukulia suala hilo ‘personal’ kwakuwa yaliyofanyika ni mambo ya kisheria tu.
Kwa upande wake AY amedai kuwa kwenye mazungumzo hayo TCRA imemshauri kurekebisha baadhi ya sehemu zenye matatizo katika video hiyo ili ianze kuchezwa tena kwenye TV muda wowote.
Post a Comment