JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi eneo la masaki jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tatu eneo Masaki Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kamishina Sirro amesema kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa wakati wakiwa wanajiandaa kufanya tukio la uhalifu katika moja ya ofisi ya kubadilisha fedha za kigeni iliyopo Masaki.
Amesema kuwa watu hao walikuwa katika gari lenye namba za usajili T 135 AQJ aina ya Rav 4 rangi ya Silver, polisi walilisimamisha gari hilo ndipo majambazi hao wakaanza kurusha risasi na kisha kuzidiwa na kuuawa na polisi waliokuwa katika doria.
Amesema baada ya kuwaua majambazi hao walikwenda kukagua na kukuta bunduki mbili aina ya pisto, Hirizi, Bomu la Kurusha na Mkono pamoja na karatasi ambayo ilikuwa imeandikwa maneno ya kiaraabu. Sirro amesema ametangaza kiama kwa watu wanaotumia nguvu katika utafutaji fedha kuwa hawana nafasi tena katika jiji la Dar es Salaam.
Aidha amesema kuwa mwandishi, Salma Said aliyetekwa Zanzibar hivi karibuni ni mzima kutokana na kumkuta kuwa hana jeraha lelote katika mwili wake.
Amesema kuwa mwandishi huyo wamechukua malalamiko ambapo wanafanyia upelelezi juu maelezo aliyetoa baada kuonekana katika mazingira hayo.
Aliongeza kuwa baada ya upelelezi watachukua hatua lakini kwa sasa yuko katika matibabu katika Hospitali ya Regency Jiijini la Dar es Salaam.
Post a Comment