Mamlaka ya Reli Nchini (TRL) imesitisha safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Mikoani na kuhamishia huduma hiyo mkoani Dodoma kutokana miundombinu ya reli kuharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Mvua hizo zimeharibu miundombinu ya reli ya kati wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Kaimu Mkurugenzi TRL, Masanja Kadogosa amesema kuwa kutokana na kusitishwa kwa huduma hiyo ratiba ya huduma mpya inatarajiwa kuanza kesho Machi 22 kwa wasafiri wanaotarajia kusafiri kutoka Dodoma kwenda Mwanza na Kigoma kuanzia majira ya saa 11 jioni.
Amesema gari moshi jipya ya Delux kwa wasafiri wa Kigoma wanatakiwa kukata stakabadhi ya malipo ya safari siku ya Jumanne saa 2:00.
Kadogosa amesema kuwa jitihada mbalimbali zinaendelea kufuatia mashirikiano kati ya kampuni hodhi ya Rahco pamoja na Shirika la reli nchini ili kuweza kurejesha huduma hiyo kama ilivyokuwa awali.
Amesema kuwa wasafiri wanaotumia usafiri huo waondowe wasiwasi kutokana na jitihada zinazofanywa za urejeshaji wa huduma ya reli.
Post a Comment