Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SAID FELLA AJIPANGA KUWANIA URAIS WA NCHI


Meneja wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family Said Fella ‘Mkubwa Fella’ anajipanga kuogombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2040 akiwa na umri wa miaka 60.

Fella ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kilungule wilayani Temeke jijini Dar es salaam (CCM), amekiambia kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumatano hii kuwa  yeye ni mtu makini,  hivyo hawezi kushindwa kuiongoza nchi.

“Kama Mungu akinipa uhai mwaka huo nitakuwa na miaka 60 na nitakuwa nina uelewa wa kutosha na uwezo wa kuweza kuwaongoza watanzania kwa kujali maslahi yao ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini” Alisema Fella.

Aidha Fella ametamba kuwa yeye anafanya kazi kwa vitendo ndiyo maana wananchi wa kata yake walimuamini na katika madiwani wote wa Dar es salaam yeye ndiye diwani pekee aliyeshinda kwa asilimia 89% katika uchaguzi mkuu wa October 2015.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright 2025 EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG | Designed By Code Nirvana