Baadhi ya Wabunge wa Ukawa wakiwa katika ofisi za Mkurugenzi wa Jiji
Wawakilishi hao wa wananchi wanaeleza kwamba, hawapo tayari kuondoka kwenye ofisi hizo mpaka Willison Kabwe ambaye ndiye mkurugenzi wa jiji hilo awaelezwe tarehe ya uchaguzi huo.
Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dr es Salaam umekuwa mwiba kwa Ukawa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo wameendelea kuvutana na kusababisha kuhairishwa mara nne sasa.
Tayari uchaguzi huo umesababisha baadhi ya wabunge na madiwani jijini humo kufikishwa mahakamani kwa madai ya kuwa chanzo cha vurugu na kuahirishwa kwa uchaguzi huo ulioitishwa Jumamosi iliyopita.
Wabunge hao ni Halima Mdee wa Jimbo la Kawe pamoja na Waitara Mwita, Mbunge wa Ukonga ambao kwa sasa wamepo nje kwa dhamana.
Tayari Ukawa jijini Dar es Salaam wamemgomea Meck Sadick, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kushiriki Kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) Mkoa wa Dar es Salaam kwa madai ya kutotendewa haki.
Wabunge hao waliandikiwa barua na Theresia Mmbando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwaarifu wabunge hao pamoja na wajumbe wengine wa kikao hicho kushiriki na baadaye kwenda kutembelea miradi ya maendeleo.
Mmbando ndiye liyekuwa Mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika Jumamosi wiki iliyopita na baadaye kuhairishwa na kuibua malumbano ya kisiasa.
Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam umeendelea kughairishwa kutokana na kuibuka vuta nikuvute kati ya Ukawa na CCM huku ikitajwa kwamba, CCM wanaendesha hujuma ili kutwaa nafasi hiyo licha ya kuwa wachache.
Miongoni mwa wabunge waliogomea kikao hicho ni pamoja na Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema); Abdallah Mtulea, Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF); Maulid Mtulia, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni (CUF) na Waitara Mwita, Mbunge wa Ukonga (Chadema
Post a Comment