Matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo yamekuwa yakiongezeka kwa kiwango kikubwa, ongezeko hili limebainika kutokana na ufuatiliaji tulioufanya kupitia matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi ambapo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2016 kumeripotiwa matukio 1765 ukilinganisha na matukio 1585 katika kipindi kama hicho mwaka 2015 ikiwa ni ongezeko la matukio 180.
Katika
matukio ya Januari hadi machi 2016, jumla ya watuhumiwa 823 wamekamatwa
na kufikishwa mahakamani ingawa bado kumekuwa na tabia ya wazazi na
walezi kuficha watuhumiwa wa ubakaji na kumaliza kesi hizo kirafiki au
kifamilia jambo ambalo ni kinyume cha sheria bila kuzingatia madhara
aliyoyapata mtoto.
Kufuatia
hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linakemea vikali wale wote
wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu vya ubakaji na wazazi ama walezi
wanaofumbia macho vitendo hivyo na kuingia makubalino na watuhumiwa kwa
kupeana fedha kama fidia ili wamalize kesi kiundugu au kifamilia.
Jeshi
la Polisi linatoa wito kwa Wazazi, walezi, Viongozi wa dini, Asasi za
kiraia, walimu na Wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano katika
kushughulikia vitendo hivyo ikiwemo kuwafichua wazazi au walezi
wanaofanya makubaliano ya kumaliza kesi za ubakaji kirafiki au kifamilia
ili kukomesha vitendo hivyo.
Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Post a Comment