Bi.Yasmin
Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle
cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam. Mama huyu ambaye mwanaye pia anaugua ugonjwa huo,
lakini matibabu yake anapatanchini Uingereza, ameamua kusimama kidete
kutetea wagonjwa wa selimundu kuendelea kuhudumiwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili, na kumuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuingilia kati
mpango wa kuwaondoa wagonjwa 6,000 hospitalini hapo na kuwapeleka kwenye
hospitali wanakotoka.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, MNH
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili, MNH, na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa
Jamii, Wazee na Watoto, wametoa msimamo kuhusu sintofahamu iliyowakumba
wagonjwa wa sickle cell (Selimundu), waliokuwa wakipatiwa matibabu
kwenye hospitali hiyo kubwa kabisa hapa nchini.
Kauli ya MNH kuhusu tiba ya Selimundu
“Tunapenda
umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala Hospitali
haitasitisha utoaji wa huduma hiyo.” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali
hiyo, Profesa Lawrence M. Museru, amewaambia waandishi wa habari leo
Aprili 25, 2016.
Hofu ya wagonjwa
Awali
baadhi ya wazazi wa watoto wenye kuugua maradhi ya Selimundu,
wakiongozwa na Bi.Yasmin Razak, wameonyesha hofu ya maisha ya watoto wao
kufuatia taarifa kuwa jumla ya wagonjwa 6,000 waliokuwa wakipatiwa
matibabu ya Selimundu hospitalini hapo chini ya mradi wa utafiti wa
ugonjwa huo, “Welcome Trust.” Watarudishwa kwenye utaratibu wa matibabu
chini ya muongozo wa Wizara ya Afya kwenye hospitali walikotoka, kwa
vile mradi huo wa utafiti umemaliza kazi yake Machi 31, 2016.
Gharama za matibabu ya Selimundu
Ni kweli
kwamba takribani miaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili
matibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa wa selimundu, Mradi huu kwa
sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote wa selimundu kuja Muhimbili
kwa ajili ya utafiti na tiba. Hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwa
wengi wanaohitaji huduma ya selimundu kuja Hospitalini hapa licha ya
kwamba mahitaji yao hayakuhitaji utalaamu wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili,
Amesema Profesa Mseru.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dkt.Doroth Gwajima,
amewaondoa hofu wagonjwa kuhusu gharama za matibabu hayo ambapo alisema,
muongozo wa serikali uko wazi, wazee na watoto watapatiwa matibabubure
na wengine wanachangia kupitia bima ya afya na fedha taslim, hata
hivyokwa wale ambao hawatakuwa na uwezo utaratibu wa kuwapatia matibabu
upo.
Hofu ya wagonjwa
Kutokana
na mazoea ya muda mrefu ya kupatiwa matibabu bure ya ugonjwa huo wa
selimundu, na hasa ikizingatiwa hakuna tiba ya kuuponya kabisa ugonjwa
huo, wagonjwa wamehoji watawezaje kumudu kulipia gharama hizo?
Wazazi wa
watoto wanaougua ugonjwa huo, wametmuomba Rais John Magufuli, kuingilia
kati suala hilo ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao ambao kwa asili ya
ugonjwa wenyewe, mgonjwa hupata maumivumakali mwilini, mabadilikoya
viungo, na wakati mwingine kupungukiwa damu mara kwa mara.
Kauli ya Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
“Hospitali
zote za Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, na hata zile zilizopo
mikoani na wilayani, zina uwezo wa kutoa huduma za ugonjwa wa Selimundu,
na hata ikionekana kuwa mgonjwa anahitaji matibabu zaidi, rufaa
huandaliwa na mgonjwa hupelekwa kwenye hospitali kubwa zaidi ili
kupatiwa matibabu yanayofaa.” Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la
Dar es Salaam.
Bi.Getrude Thadeo kutoka Tabora, akiwa na mtoto wake wa miaka 13, Angela Romwadi, ambaye anaugua Selimundu
Bi.Mkami Titus wa Temeke jijini Dar es Salaam akiwa na mtoto wake Shedrack Yahaya(4), anayeugua selimundu
Bi.Walivyo Mohamed kutoka Rufiji mkoani Pwani, akiwa na mtoto wake wa miaka 4, Siraji Majid
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitaliya Taifa Muhimbili, (MNH), Profesa Lawrence
Museru, (kulia), akiwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa na Afya ya Watoto ya
MNH, Dkt. Mary B. Charles, akizungumza na waansdishi wa habari wakati
akitoa taarifa yake mapema leo Aprili 25, 2016
Profesa Museru
Dkt.Doroth Gwajima, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
Profesa Museru natimu yake wakati akiongea na waandishi wa habari
Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt.
Elineema Meda. Dkt. Meda ni mmoja wa walioshiriki kwenye utafiti wa
ugonjwa huo wa Selimundu chini ya mradi wa Welcome Trust
Bi. Yasmin wakati wa mkutanona waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Baadhiya
akina mama wakiwa na watoto wao wanaosumbuliwa na maradhi ya Selimundu.
Hapa wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Bi.
Yasmin ambaye ameamua kuwasimamia na kuwasemea wagonjwa wa Selimundu
Bi. Yasmin (katikati), akiwa na Bi.Walivyo Mohammed na mtoto wake Siraji (kushoto) na Bi. Getrude Thadeona mtoto wake Angela
Post a Comment