Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kijeshi wa serikali ya China na Tanzania katika hafla ya Meli ya Kivita ilivyowasili jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing katikati ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa Wananchi,Meja Jenerali Venance Mabeyo wakati hafla ya Meli ya Kivita ilivyowasili jijini Dar es Salaam.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi wa Wananchi, Meja Jenerali Venance Mabeyo akizungumza juu ya ushirikiano wa Tanzania na China katika kubadilishana uzoefu wa kijeshi hafla ya Meli ya Kivita ilivyowasili jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
KUTOKANA na kuwepo kwa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali katika bahari ya hindi kumesababisha serikali kukosa mapato yatokanayo na kodi ,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameomba msaada wa boti kwa serikali ya China kwa ajili ya kufanya doria katika fukwe za bahari za jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa katika hafla ya ziara ya Meli za Kivita ya China iliyozuru jijini Dar es Salaam, Makonda amesema kuwa boti zikiwepo zitasaidia kufanya doria katika bahari ya hindi na kuweza kuua mtandao wa usafirishaji biashara zinazosafirishwa kwa boti kushushwa katika fukwe na kuingia mtaani.
Amesema licha kuwepo kwa usafirishaji wa bidhaa katika bahari ya hindi kuwepo usafirishaji bidhaa lakini kuna matukio ya uhalifu yanafanyika hivyo boti za doria zitafanya kazi na kuweza kukomesha uhalifu huo.
Makonda amesema ujio boti huo utaendana na kuja kwa askari 300 wa China ambao watatoa mafunzo kwa askari wa Tanzania kuweza kutumia boti hizo pamoja na mbinu za kufanya doria za kuweza kuweakamata wahalifu wote katika fukwe zote.
Aidha amesema kuwa doria hizo zitakwenda sambasamba na ndege ndogo pamoja na gari maalumu za kufanya doria hiyo kwa wale wanaokamatwa kuwekwa katika gari hizo.
Post a Comment