Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAANGALIZI WA KIMATAIFA WA UCHAGUZI TOKA EU WAFUNGUKA MAZITO JUU YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25, 2015

Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015, leo umewasilisha ripoti yake kamili iliyo na mapendekezo ya marekebisho ya kuboresha mchakato wa uchaguzi na kuongeza imani juu ya chaguzi zijazo, kwa washirika wake nchini.

Uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015, uliyofanyika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ulionyesha dhamira ya Watanzania ya kuzingatia mfumo wa kikatiba na pia kuheshimu misingi ya kidemokrasia.

Chaguzi zote mbili za tarehe 25 Oktoba, yaani za Muungano na Zanzibar, zilikuwa na ushindani mkali na kwa kiasi kikubwa ziliendeshwa vyema. Taasisi za usimamizi wa uchaguzi zilionyesha viwango vya kutosha vya kujiandaa pamoja na uwezo wa kuendesha hatua muhimu katika kuandaa uchaguzi, kuelekea na pia siku ya uchaguzi.

Kulikuwepo, hata hivyo, na mapungufu kadhaa yanayopaswa kuangaliwa kuhusu mfumo wa kiuchaguzi pamoja na utendaji wa mchakato wa uchaguzi kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Zaidi ya hayo, taasisi za usimamizi wa uchaguzi hazikuonyesha uwazi kamili juu ya michakato yao ya kufanya maamuzi.

Tathmini chanya juu ya kuaminika kwa uendeshaji wa uchaguzi siku ya uchaguzi ilihusu pia Zanzibar. Kufuatia uamuzi wa ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar, EU EOM pamoja na waangalizi wengine wa kimataifa, katika tamko la pamoja, walielezea wasiwasi wao mkubwa na kuiomba ZEC iwasilishe ushahidi wa kuhalalisha uamuzi huo ambao haujawahi kutokea.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top