Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Emmilius Mchauru wa kufuta shtaka la kutakatisha Dola Milioni 6 za Kimarekani baada ya kuona liliondolewa kinyume cha sheria!
Kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (pichani kati) Harry Kitilya na wenzake dhidi ya mashtaka manane ikiwamo la kutakatisha fedha na walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi Mwaka huu.
Akisoma uamuzi huo Jaji Edson Mkasimongwa alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili mahakama yake imeona Hakimu Mchauru wa Mahakama ya Kisutu alikosea kuliondoa shtaka hilo na kwamba shtaka la kutakatisha fedha litabaki kama lilivyofunguliwa katika hati ya mashtaka.
"mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria kulifuta shtaka la 8 na ninaamuru kurejesha kumbukumbuku ya jalada la kesi hii kwa ajili ya kuendelea kusikilozwa" alisema Jaji Mkasimongwa.
Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania 1996 Shose Sinare na Sioi Solomon ambao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mchauru.
Awali, jopo la mawakili wa utetezi liliwasilisha maombi ya kuliondoa shtaka la nane ya kutakatisha fedha na mahaka?a ya Kisutu ilikubali na kuliondoa.
Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Osward Tibabyekomya ulowasilisha nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam alitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwamba mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza rufaa ya kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha.
Upande wa Jamhuri ulikata rufani katika Mahakama ya Rufani Tanzania.
Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jopo la Majaji watatu ikiongozwa na Bernad Luanda,Salum Masati na Aristoclas Kaijage liliamuru jalada la kesi hiyo kurejeshwa mahakama kuu na kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufaa ya Jamhuri.
Jalada hilo lilipangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mkasimongwa.
Post a Comment