Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MPYAAA!! Mawakili wa Chadema chali, zuio la maandamano pale pale

SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutangaza kuitisha maandamano ya nchi nzima, uamuzi huo umepata pigo baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mbali ombi lao la kutaka kutengua amri ya Jeshi la polisi.

Hii ina maana, kisheria, amri ya zuio iliyowekwa na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa (yasiyo na kibali) inabaki kuwa halali na kusanyiko au maandamano yoyote yasiyo na kibali cha Jeshi hilo ni haramu.
Wameanguka


Uamuzi huo pia umewabwagwa mawakili wa Chadema wakiongozwa na Peter Kibatala ambaye siku zote anaposhinda kesi moja bila kujali uzito na mazingira ya ushahidi hujinasibu kuwa wakili bora kuliko wengine.

Kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Dar es Salaam jana na Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali, ombi la Chadema kutaka amri ya IGP kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima ya vyama vya siasa na maandamano “limeangukia pua” kutokana na mawakili wa Serikali kuweka hoja nzito kupinga ombi hilo.

Mawakili wa Serikali Haroun Matagane, David Nyakia na Lilian Machage waliwasilisha hoja mbili za kisheria dhidi ya ombi la Chadema lililowasilishwa na Wakili Peter Kibatala.

Kutokana na Mahakama kukubaliana na hoja nzito za kisheria za Mawakili wa Serikali katika kesi hiyo na 52 ya mwaka huu, waleta maombi katika kesi hiyo ambao ni wadhamini wa Chadema wameamriwa pia kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Na Anna Msina, Blogu ya Sheria, Dar es Salaam
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top