Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia leo wamewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Bukoba. Pia waliambatana na Mbunge wa Viti Maalum Bi. Savelina Mwijake, Mbunge wa Bukoba Mjini, Mh. Rwakatare pamoja na Viongozi mbalimbali.
Mhe. James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi ambae ni Mtaalamu wa Masuala ya Maafa amewaunga mkono Wanabukoba leo akiambatana na Mwenyekiti mwenza Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe kwenye safari ya kuwatembelea wahanga. Katika Safari hiyo wametoa misaada ya dharura kwa wahanga ikiwemo chakula, sukari, fedha na n.k, wataendelea na safari hiyo kuwatembelea Wahanga hapa Mkoani Kagera katika sehemu mbalimbali. Leo wametembelea sehemu ya Kibeta, Hamugembe, Kashozi, Nshambya katika shule ya Ihungo iliyoathiriwa zaidi na Tetemeko hilo kubwa la Ardhi na kuwafanya wanafunzi kusimamisha masomo yao kwa wiki mbili kwa kukosa sehemu ya kusomea/Madarasa na Mabweni.
Sehemu ya Majengo katika Shule hiyo kwa sasa baada ya kutokea Tetemeko
Tetemeko likiwa limeharibu sana sehemu kubwa ya Kanisa katika Shule hiyo ya Ihungo iliyopo kilometa 8 kutoka Bukoba Mjini
Taswira ya sasa Wanafunzi wa Shule ya Ihungo wakijipanga kuondoka Majumbani mwao baada ya Tetemeko la jumamosi kuwaathiri kiasi kikubwa na kushinikizwa kufunga shule hiyo kwa wiki mbili kupisha kuangaliwa upya kwa Shule hiyo kutokana na kuathiriwa na tetemeko.
Post a Comment