Loading...
Spika Ndugai akabidhiwa kitambulisho cha Taifa kikiwa na saini yake
Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amekabidhiwa kitambulisho chake cha Taifa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba leo mjini Dodoma ambacho kinaonesha picha yake, saini yake pamoja na saini ya mtoa kitambulisho.
Hatua hiyo ya Spika Ndugai ya kupokea kitambulisho hicho ni mkakati wa taifa ambao NIDA imekusudia kukamilisha usajili wa vitambulisho vya taifa nchi nzima kwa wananchi, wageni na wakimbizi ifikapo Desemba mwaka huu pamoja na kutoa namba ya utambulisho ambayo itawezesha makundi yote kupata huduma mbalimbali.
Chanzo: Mwananchi
Post a Comment