Loading...
RIPOTI YA TWAWEZA: WANANCHI WAYAKATAA MAIGIZO YA KINA MBOWE, WAMKUBALI JPM
Josina Anaclet, Dar
ASILIMIA 96 ya wananchi wanaukubali uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano, Dkt John Pombe Magufuli.
Kwa mujibu wa utafiti uliotolewa Septemba 15 na taasisi ya Twaweza, wananchi hao wameonesha kuridhishwa zaidi na jinsi Rais anavyopambana kuondoa watumishi hewa, kupambana na ufisadi na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wasiofuata maadili.
Utafiti huo unaohusisha maoni ya wananchi kwa njia ya simu kutoka katika kaya zao unadhihirisha kuwa licha ya wapinzani kuhaha kubeza staili ya Rais, wananchi wanaangalia zaidi maendeleo na wanaridhishwa na maono yake.
"Utafiti huu maana yake ni ndogo tu na rahisi kuielewa; wananchi wanaimani na mtazamo wa kimataendeleo wa Rais kuliko siasa siasa za kina Mbowe," anasema mtaalam wa masuala ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 Rais Magufuli alipata asilimia 58 ya kura zote.
Utafiti huu unamaanisha kuwa iwapo uchaguzi ungefanyika leo, kukubalika kwa Rais Magufuli kungekuwa kwa kiwango cha juu zaidi.
"Wananchi wamebadilika sana hasa vijijini.Wakati vijana mijini wanamezwa na siasa na kujiongezea umaskini, vijijini wananchi wanapokea na kukubali utendaji wa viongozi na wanapata maendeleo makubwa kwani miradi mingi inatekelezwa huko kwa sasa," anasema mtaalamu mmoja wa siasa.
Hata hivyo yako maeneo wananchi wameona uamuzi wa Serikali ulihitaji kufanyiwa kazi kabla kama vile suala la sukari.
Taarifa kamili ya Twaweza inapatikana hapa
http://twaweza.org/index.php?i=1441
Post a Comment