Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ubuyu mpyaaa ... Linah, Idrisa Sultan ndani ya penzi zito

IMEBUMBURUKA! 
Sexy lady wa Bongo Fleva, Estalina Sanga ‘Linah’ na Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan, wanadaiwa kuwa ndiyo habari ya mjini kwa sasa kwani penzi lao siyo siri tena. Kwa mujibu wa sosi wa karibu wa mastaa hao, kwa sasa penzi lao halina kificho kwani wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali baada ya uvumi wa muda mrefu kuwa wana uhusiano lakini wakawa wanaficha.

MAMBO YALIVYOANZA. 
Uvumi wa Linah na Idris ulianza mwezi uliopita baada ya ubuyu kuzagaa kuwa mrembo huyo aliwahi kuonekana nyumbani kwa Idris, kitendo kilichozua maswali kwamba alikwenda kufuata nini. Katika uvumi huo, baadhi ya watu walidai kuwa uhusiano wao ulikuwa umeanza chinichini baada ya Idris kumwagana na Wema Isaac Sepetu.

KISA CHA PENZI HILO CHATAJWA 
Sosi huyo aliiambia Chobingo ya Ubuyu kuwa, chanzo cha Linah kuingia kwenye uhusiano na Idris ni kulipa kisasi kwa Wema aliyewahi kuingilia uhusiano wake na mpenzi wake wa zamani, Nagar Kombo aliyetoka na Wema wakati Linah akiwa bado kwenye uhusiano naye.

WIKIENDA KAMA KAWA 
Baada ya ubuyu huo kufika kwenye Meza ya Wikienda, mwanahabari wetu alimwendea hewani Idris aliyekiri Linah kufika nyumbani kwake lakini akadadavua kwamba alikwenda kwa sababu ya ushkaji tu na hakuna kilichoendelea. Majibu hayo Idris aliyatoa mwezi mmoja uliopita yalikanushwa juzikati baada ya kusambaa kwa picha ikimuonesha akiwa na Linah kwa karibu kiasi kwamba kwa mtu mwenye akili zake, hakuwa na sababu ya kuambiwa kuwa mastaa hao wanatoka kwani kila kitu kilijieleza.

BETHIDEI YA BEN POL
Wakati hayo yakiendelea, wikiendi iliyopita, wawili hao walinaswa laivu wakijibebisha kwenye bethidei ya staa wa RnB Bongo, Benard Paul ‘Ben Pol’ iliyofanyika kwenye Klabu ya Next Door, Oysterbay jijini Dar hivyo kushibisha madai kuwa kuna kitu kinaendelea kati yao. Pia fukunyuafukunyua za Ubuyu zilitembelea kwenye ukurasa wa Linah na kubaini kuwa amekuwa akimposti Idris na kuweka maneno ya kejeli huku akidai kuwa hamuogopi mtu zaidi ya Mungu.

 UJUMBE HUO ULISOMEKA HIVI:
 “Kama Mungu alitupenda sote! Why na sisi tusipendane? Raha jipe mwenyewe babu, nafanya ninachojisikia na siyo unachojisikia, simuogopi yeyote zaidi ya Mungu tu, kijani haiwezi kuwa nyekundu hata iweje.

” BOFYA HAPA KUMSIKIA LINAH 
Wikienda lilipomtafuta Linah ili kumsikia anasema kuhusu uhusiano wake na Idris, mambo yalikuwa kama ifuatavyo; Wikienda: Ishu na wewe kutoka na Idris ikoje? Linah: “Hahahaaa…(kicheko hadi kilio). Kwani kuna mtu kati yetu kasema tuna uhusiano? Sisi mbona ni marafiki wa kawaida? Wikienda: Ndiyo habari ya mjini na mitandaoni kumechafuka. Pia mwezi uliopita ulionekana nyumbani kwake na hilo likoje? Linah: Kha! Wikienda: Kwani hujaona Team Wema wanavyokutukana? Linah: Sikia, hakuna kati yetu aliyesema kama kuna uhusiano ‘so’ mimi nafikiri acha waendelee kutukana. Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wao waliupongeza uhusiano wa mastaa hao lakini wapo waliouponda kwa kigezo kwamba kitendo cha mastaa kuchukuliana ‘mabwana’ si cha kushadadiwa.

NENO LA MHARIRI    
Kama kweli Linah ameamua kutoka na Idris kwa maana ya kulipa kisasi, kitendo hicho ni cha aibu kwani kila kukicha mastaa wamekuwa wakibadilishana mabwana kwa maana ya kulipa kisasi lakini mwisho wa siku wanaweza kujikuta wakiambukizana magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi na kuishia kujuta.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top