Anaandika Mh. Saed Kubenea (Mb)~UBUNGO.
--------------------------------------------------------------
Hatimaye ile Kesi ya uchochezi iliyokuwa ikinikabili, imefutwa na mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu. Katika shauri hilo, serikali ilidai kuwa niliandika habari za uchochezi katika gazeti la MwanaHALISI juu ya kilichotokea Unguja na Pemba, baada ya kufutwa kwa uchaguzi huru na haki wa 25 Oktoba mwaka 2015.
Katika uamuzi wake huo, Hakim Mashauri alikubaliana na hoja za utetezi na kuamuru kuniachia huru. Hata hivyo, mara baada ya kuniachia huru, jeshi la polisi limenikamata na niko kituo cha polisi kati.
Naombeni dua zenu.
Saed Kubenea(Mb)
on Wednesday, January 25, 2017
Post a Comment