Dar es Salaam. Katibu wa waumini wanaomuunga mkono Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya, Thomas Gambo amesema kinachompa kiburi Dk Valentino Mokiwa ni kuungwa mkono na baadhi ya mapadri, makasisi na mashemasi ambao aliwawekea mikono akiwa askofu wa Dayosisi ya Dar es Saalam.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake jana, Gambo alisema Dk Chimeledya atafanya ibada ambayo itahusisha kumsimika Naibu Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, itakayoamua mustakabali wa mgogoro wa uongozi uliopo.
Ibada hiyo itafanyika Kanisa Kuu la Dar es Salaam. Hata hivyo, hawakutaja siku bali alisema katika ibada hiyo, Askofu Chimeledya atafanya mambo mbalimbali ikiwamo kutangaza kubadilisha uongozi wa dayosisi na kuwapa upya viapo mashemasi na mapadri.
Dayosisi ya Dar es Salaam imekuwa katika mgogoro tangu Askofu Chimeledya amtake kiongozi wake, Dk Mokiwa ajiuzulu kwa madai kuwa anatumia madaraka yake vibaya na tuhuma za ubadhirifu.
Hata hivyo, Dk Mokiwa alikataa kujiuzulu, akisema mkuu wake alikiuka taratibu ikiwamo kufanya uamuzi ambao uko chini ya mamlaka ya dayosisi na kutopeleka uamuzi huo kwenye Nyumba ya Maaskofu kama taratibu zinavyotaka.
Gambo alisema: “Siku hiyo tutawajua mashemasi na mapadri wanaomuunga mkono Askofu Chimeledya na Dk Mokiwa.”
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
THBUB YACHUNGUZA MAUAJI YA KIUNGONI, PEMBA6 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment