Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya kukamatwa kwa jumla watuhumiwa 349 katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaohusika na dawa za kulevya
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao, wamo wauzaji, wasafirishaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na kwamba wataanza kufikishwa mahakamani siku ya kesho, huku mmoja akipandishwa kizimbani leo.
Pia ametoa taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za uongo, ambapo amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia kijana huyo ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya viongozi na kuwatuhumu kuwa wanahusika na dawa na dawa za kulevya.
Kuhusu askari 9 waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, Kamanda Sirro amesema askari hao wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda Sirro amesema hadi sasa jumla ya kete 612 pamoja na bangi vimekamatwa na kwamba kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo linawafuatilia na watakuwa mbaroni wakati wowote.
Post a Comment