Mgeni rasmi akiwa waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage wa tatu kushoto,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanga cha utengenezaji wa viungo,Vegata Podravka Ltd,kilichojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 16,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo,Mh.Shukuru Kawambwa na kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croati,Bi..Olivia Jakupec
waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea akipata maelekezo mbalimbali kuhusiana na baadhi ya bidhaa ambazo ziko tayari kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croati,Bi..Olivia Jakupec.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd,Bw-Tanzania,.Davor Svar akizungumza kwa ufupi wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha viungo mbalimbali,jana mjini Bagamoyo,huku mgeni rasmi akiwa waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
Davor alisema kuwa wameamua kuwekeza nchini Tanzania kwa sababu imeonekana ni kiungo muhimu katika mambo ya uwekezaji hasa kutokana na eneo lake, miundo mbinu yake,ukuaji wake wa kiuchumi na pia kuwa kiungo muhimu kwa kuwa mwanachama hai wa nchi za Afrika Mashariki na Kati,kufuatia vigezo hivyo,hurahisisha mambo ya kibiashara kufanyika kwa urahisi zaidi.
Davor alisema kuwa kufuatia kuanzishwa kwa kiwanda hicho,kimefanikiwa kutoa ajira za kazi zaidi ya 200 katika Wilaya ya Bagamoyo ikiwemo kazi ya uuzaji na usambaji wa bidhaa za kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd-Tanzania,Davor Svar akifafanua jambo kwa Mgeni rasmi,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage,kabla ya hafla fupi ya uzinduzi wa kiwanda hicho,uliofanyika mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha utengenezaji wa viungo mbalimbali,mjini Bagamoyo mkoani mkoani Pwani.
Olivia alisema kuwa wao kama wawekezaji wametembea nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Uganda,Kenya,Burundi,Zambia,Rwanda,Sudani Congo,Afrika Kusini na nyinginezo,lakini wakabaini Tanzania ndio mahali sahihi kwa uwekezaji."Hivyo tukafanya utafiti,tukabaini eneo la Bagamoyo linafaa kujengwa kiwanda cha aina hiyo,hivyo tukaamua kujenga kiwanda ndani ya mwaka mmoja na nusu,ambacho kimetumia kiasi cha shilingi bilioni 16 mpaka kukamilika.
"Tunaishukuru Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Waziri wa Viwanda Mh.Charles Mwijage,Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wengineo kwa ujumla, kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji,kiasi kwamba hata nasi tukaiona furasa hiyo na tukachukua hatua ya kuwekeza kiwanda hiki hapa nchini",alisema Olivia.
Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kiwanda cha Viungo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho wilayani Bagamoyo,Pwani.Waziri Mwijage alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano imeamua kujenga Uchumi wa Viwanda,ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya Watu.
"Tanzania sasa tunajenga viwanda na si Tanzania ya viwanda inawezekana,hiyo ilikuwa kauli mbiu ya zamani,kwa hiyo sasa tunajenga viwanda,mwenye macho haambiwi Tazama"alifafanua Waziri Mwijage.Waziri Mwijage amewashuruku wawekezaji hao kwa kuamua kuja kuwekeza nchini Tanzania,ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano ,Dkt John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Uchumi wa Viwanda unakwenda kwa kasi na kufanikiwa.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd,Bw-Tanzania,.Davor Svar mara baada ya kusoma hotuba yake iliyowahamasisha wakati wa Wilaya ya Bagamoyo kuchangamkia fursa mbalimbali zitokazo na ujenzi wa viwanda vya aina mbalimbali vinavyoendelea kujengwa wilyani humo mkoani Pwani.
Sehemu ya meza kuuu
Wageni waalikwa kutoka kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri
Baadhi ya wageni waalkwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akimkabidhi Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage cheti cha heshima ya ushiriki wake mkubwa katika uzinduzi wa kiwanda hicho
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akimkabidhi Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage cheti cha heshima ya ushiriki wake mkubwa katika uzinduzi wa kiwanda hicho.Pichani kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd-Tanzania,Davor Svar
picha ya pamoja
Picha pamoja
Baadhi ya Wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) wakipewa maelezo mafupi namna ya bidhaa hizo zinavyotengenezwa kiwandani hapo
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na usindikaji wa viungo kiwandani humo
Credit: Jiachie Blog
Credit: Jiachie Blog
Post a Comment