Loading...
SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA ... Mbowe agoma kwenda Polisi .... Atoa tamko zito
KAULI YA MH. FREEMAN AIKAEL MBOWE KUHUSU SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA.
Mbowe anazungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma hivi sasa hivi
Amekanusha vikali tuhuma za kuhusika na biashara au kutumia madawa ya kulevya.
Anasema wao kama chama wanaunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Anasema kua serikali imechelewa kuendesha vita hiyo.
Asema Chadema na kambi ya upinzani kwa ujumla haiungi mkono mapambano hayo yanayoendeshwa kwa hila.
Mbowe asema RC hana mamlaka ya kisheria ya kumuita mtu Polisi.
Anasema RC anachofanya ni kuwaepusha watuhumiwa wa dawa za kulevya na mkono wa sheria
Anasema atamfungulia mashitaka ya kumchafulia jina lake kwa kumhusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Anasema yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote endapo njia sahihi zitatumika.
Post a Comment