HISTORIA YA JESHI LA POLISI – TANZANIA
1885; Wajerumani walifika Tanganyika ili kutawala, waliunda kikundi cha watu kilichofanya kazi ya Polisi.
1916; Vita kuu ya kwanza ikiendelea Ulaya na Afrika, kundi la Maafisa 31 (NCO) kutoka Afrika Kusini wakiwa na silaha (Rifle) walifika Tanganyika kufanya kazi za Polisi.
1919; Tarehe 25 August 1919 Serikali ya Kiingereza ilitangaza katika Gazeti la Serikali No.Vol.1 No.21-2583 kuwa Jeshi la Polisi Tanganyika limeanzishwa rasmi. Makao Makuu ya Jeshi hilo yalikuwa Wilayani Lushoto chini ya uongozi wa Major S.T DAVIS.
1921; Kundi lingine la Wakaguzi kutoka Ulaya lilifika nchini Tanganyika kuanzisha shule ya Mafunzo ya Polisi huko Morogoro.
1925; Kituo cha kwanza rasmi cha Polisi nchini kilifunguliwa huko Lupa Tingatinga kwenye machimbo ya dhahabu Chunya.
1930; Makao Makuu ya Polisi yalihamishwa kutoka Lushoto kuja Dar es Salaam.
1949; Motorized Company sasa Field Force Unit (F.F.U) kilianzishwa nchini kurejesha amani penye vurugu.
1949; Vijana mbalimbali wa Kiafrika toka shule mbalimbali za Sekondari Nchini walichaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi na kuwa Wakaguzi chini ya uangalizi (Probation Inspectors).
1952; Kikosi cha Mawasiliano (Signals Branch) kilianzishwa katika Polisi bila kutumia nyaya za simu.
1958; Askari wa Polisi wa Kikie (Women Police) walijiunga na Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa Miss. Payee.
1961; Tarehe 9 Desemba, 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake. Baada ya uhuru, Jeshi la Polisi lilianza kubadili mwelekeo toka katika kutumikia Wakoloni na Walengwa wakawa ni Wananchi kwa mujibu wa sera za Serikali ya Wananchi.
1962; Kwa mara ya kwanza nafasi ya Kamishna wa Polisi aliyekuwa Mzungu Mr. M.S Wilson – C.P, ilichukuliwa na Mwafrika
Mr. Elangwa Shaidi – C.P.
1962; Maafisa 10 Waafrika waliteuliwa kuchukua nafasi za wakuu wa Polisi wa Mikoa (Regional Police Commanders).
1964; Tarehe 26/04/1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na hivyo kuunda Tanzania. Kwa hiyo Mr. Elangwa Shaidi alipandishwa cheo nakuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP).
Alisaidiwa na Makamishna watatu wa Polisi ambao ni:-
1. Mr Edington Kisasi Kamishna wa Polisi Zanzibar
2. Mr. Hamza Azizi Kamishna wa Polisi Bara.
3. Mr. Akena Kamishna wa Polisi CID.
VIONGOZI WA JESHI LA POLISI WAKATI WA UKOLONI HADI UHURU.
1916 – 1920 Major S.T. Davis.
1920 – 1929 E.F. Brown.
1929 – 1933 G.H. Kiram.
1933 – 1942 F.A.B. Nicholl
1942 – 1949 E.B. Birthray.
1949 – 1951 W.A. Muller.
1951 – 1958 R.E. Fouler.
1958 – 1962 G.S. Wilson.
1962 – 1964 E.N. Shaidi.
MAINSPEKTA JENERALI WA JESHI LA POLISI TANGU MUUNGANO HADI LEO.
1964 – 1970
Elangwa N. Shaidi
1970 – 1973
Hamza Azizi.
7/8/1973 – Aug 1975
Samweli H. Pundugu.
8/8/1975 – Nov 1980
Philemon N. Mgaya.
2/11/1980 – 30/11/1984
Solomoni Liani.
1/12/1984 – 3/5/1996
Harun G. Mahundi.
4/5/1996 – 2/3/2006
Omar I. Mahita.
3/3/2006 - 30/12/2013
Saidi A. Mwema.
01/01/2014-Hadi Sasa
Ernest J. Mangu
WAKURUGENZI WA IDARA YA UPELELEZI (CID) TANGU 1960 HADI LEO.
- 17/9/1960 - 1/9/1961 M. J. McKinlay ACP.
- 1/9/1961 - 19/7/1962 K.F.J. Flood SSP.
- 19/7/1962 - 6/12/196 R. T. L. Egan ACP.
- 6/12/1962 - 2/8/1967 E. E. Akena ACP.
- 2/81967 - 13/11/1967 R.S. Kaswende ACP.
- 13/11/1967 - 4/6/1968 N.G.M. Sawaya SACP.
- 4/6/1968 - 2/9/1968 A.R.Shungu SACP.
- 2/9/1968 - 23/9/1970 N.G.M. Sawaya SACP.
- 23/9/1970 - 21/5/1973 S.H.Pundugu CP.
- 21/5/1973 - 28/5/1975 B.M. Omari CP.
- 28/5/1975 - 14/8/1975 F.M. Mtono SACP.
- 14/8/1975 - 15/2/1977 H.M.Lyimo CP.
- 12/2/1977 - 21/5/1981 M.Mwingira CP.
- 21/5/1981 - 6/3/1985 J.M.Lemomo CP.
- 7/3/1985 - 30/6/1992 A.A.B.Mwaitenda CP.
- 22/10/1992 - 3/5/1996 E.A.Man CP.
- 4/5/1996 - 2/3/2006 Adadi Rajab CP.
- 3/3/2006 - 14/07/2013 R.S. Manumba CP.
- 15/07/2013 - 2014 I.N. Mngulu CP
- SASA Diwan Athuman CP
Post a Comment