Mbunge wa Chalinze Mkoa wa Pwani, Ridhiwani Kikwete amehojiwa kwa muda wa saa tatu na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Ridhiwani Kikwete alitajwa katika orodha ya majina 97 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyakabidhi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.
Kiongozi huyo alihojiwa Jumatatu Machi 6, 2017 ambapo alifika katika ofisi hiyo majira ya 5:09 asubuhi akiwa amefuatana na watu wengine watatu.
Ridhiwani Kikwete baada ya kufika ofisini hapo alipelekwa kwenye chumba maalumu cha mahojiano ambapo alihojiwa kwa saa tatu ambapo inaelezwa kuwa alibainika kuwa si muuzaji wala mtumiaji wa dawa hizo, lakini tatizo ni rafiki zake ambao yupo karibu nao.
Katika taarifa yake aliyoitoa Jumanne hii, Ridhiwani amesema ameshukuru kuona haki imetendeka katika sakata hilo lililokuwa likimkabili.
“Ni kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali yangu chini ya Kamisheni ya Madawa ya kulevya inasimamia haki na nimeona ikitendeka. Niko huru toka kwenye tuhuma/kashfa,” Ridhiwani aliandika Instagram na kuongeza.
“Ni kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali yangu chini ya Kamisheni ya Madawa ya kulevya inasimamia haki na nimeona ikitendeka. Niko huru toka kwenye tuhuma/kashfa,” Ridhiwani aliandika Instagram na kuongeza.
“Tuunge mkono juhudi hizi. Tuunge mkono hatua zinazochukuliwa ili kuokoa vijana wetu na kulinda nguvu kazi ya Taifa #vitadhidiyaMadawa #magufulinikazitu #tanzaniakwanza #miminikazitu #chalinzenikazitu,”
Post a Comment