Dar es Salaam. Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema watu wote wanaoishi mabondeni watoke mara moja kwa sababu kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha na ambaye hatafanya hivyo atakamatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumanne), Siro amesema tayari amewaagiza Ma OCD na wakuu wa upelelezi kuanza oparesheni hiyo mara moja na kuhakikisha hasalii mtu katika mabonde.
Siro amesema watakaokamatwa watapelekwa polisi kwa ajili ya mahojiano kisha kupelekwa mahali ambapo wataona inafaa.
“Kuendelea kukaa mabondeni kuhatarisha maisha yako. Sisi tunadhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao hivyo hatuwezi kuruhusu kuona watu wanaendelea kufa. Tukikukuta katika mabonde yaliyokubuhu takukamata na familia yako, lazima tutumie shuruti maana binadamu wengine bila kushurutishwa hawaendi,”amesema Siro.
Loading...
Post a Comment