MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.
Maombi hayo yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.
Uamuzi huo wa majaji umefikiwa kutokana na pingamizi la jamhuri lililowasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata kuiomba kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana msingi kisheria.
Katika hatua nyingine, mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana na jopo la mawakili Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika kumtetea Mbowe.
Mbowe amefungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1, ya mwaka 2017 dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 8, mwaka huu.
CHANZO: Mtanzania
----------------
Piga ndege wawili kwa jiwe moja, ambapo utapata OFFERS mbili za kutangaza
Mosi; Kwenye blog http://www.ndgshilatu.blogspot.com ambapo litaweka kwenye USO wa blog pamoja na kurushwa Mara kwa Mara kama post ya habari.
Pili; Kama haitoshi tangazo lako tutalitangaza pia kupitia akaunti za FaceBook na Twitter za Blog hii.
Kwa kutangaza nasi biashara ama huduma yako itawafikia zaidi ya Watazamaji 50,000+ na zaidi ya nchi 120+ wanaozitembelea Blog na akaunti hizi kila siku.
Kutokana na hii ni wazi kuwa Tangazo lako litawafikia watu wengi zaidi Duniani ndani ya muda mfupi
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia e-mail pbuyegu2@gmail.com
Offer hii itadumu kwa muda mfupi tu ila tangazo lako litawekwa hewani kwa muda wa mwezi mzima.
Changamkia fursa hii adimu uimarishe Biashara yako.
on Thursday, March 2, 2017
Post a Comment