Mkurugenzi wa Vipindi na Uendeshaji wa Kituo cha Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amehojiwa leo katika kipindi cha 360 cha televisheni ya Clouds na kuthibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alivamia kituo hicho.
Ruge aliyekuwa akihojiwa na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast, Masoud Kipanya alisema alipigiwa simu na mmoja wa wafanyakazi wake kuwa Makonda ameingia ofisini hapo akiwa na polisi wenye silaha.
“Jambo hili limeniumiza sana, kwani pamoja na kuwa Makonda ni rafiki yetu lakini hatukutegemea kama angeweza kuingia ofisini na polisi wenye silaha,” alisema na kuongeza:
“Hata kama ni rafiki yako, siku moja akiingia nyumbani kwako usiku sana na silaha lazima uhoji.”
Post a Comment