Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa FFU kata ya Murriet Jiji la Arusha Anacletus Edward (CHADEMA) amejiuzulu nafasi yake, kuhama chama na kujiunga na CCM.
Akizungumza mara baada ya kujiengua Chadema mwenyekiti huyo amesema ameamua kwa ridhaa yake kujiunga na Ccm mara baada ya kuona kazi nzuri anazozifanya Rais Magufuli na serikali yake hivyo haoni haja ya kuendelea kupinga na rais.
“Kuna hoja dhaifu inayosambazwa na wenzetu kua tunawaacha kwakua tumehongwa…tunawaomba muwapuuze kwani wakati tunakuja kwao hawakusema hayo, Rais Magufuli anafanya kazi kwa maslahi ya wanyonge hivyo tuna wajibu wa kumuunga mkono na sio kumpinga” alisema Mwenyekiti huyo.
Afisa Mtendaji wa kata hiyo Joachim Kisarika amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu mwenyekiti huyo na kopi ya barua ameiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Jiji na kwa Afisa Uchaguzi wa Jiji.
Post a Comment